Willkommen auf den Partnerschaftsseiten
der HAWAKASO Songea/Tansania
und der KAB Augsburg

Button2008transp01

Wahusika CWM wa Uganda walivitembelea vikundi vya HAWAKASO huko Songea.

Georg&James02Linggen, tar. 28. 08. 2007.
George Ssozi (pichani kulia) na James Sserunjogi waliwatembea KAB huko Songea na wameripoti hali halisi ya maendeleo ya chama. Wote waili walikutana na viongozi na waliviembelea baadhi ya vikundi. Ripoti toka kwa wote wawili zinaonyesha kwamba kuna tatizo moja kubwa linalozuia uhakika wa safari ndefu na ngumu za kutembelea vikundi. Naibu wa askofu fr. Reginald Moyo, kwa mfano anatoa gari lake ili kuwezesha kuvitembela vikundi na kazi za KAB. Askofu na mapadre pia huwa wanasaidia.
Kadiri ya ripoti za wote wawili nenzo za kifedha za KAB-Songea bado ni ndogo sana na mpaka sasa bado hakuna michango ya wanachama. Ni vigumu kuwaza juu ya mipango ya fedha kama sisi tujuavyo. George na James, kwa mfano, wanatushauri kuongeza misaada ya kifedha katika kipindi hiki cha mfumuko wa bei. Kwa ajili ya uboreshaji wa mawasiliano kwa makundi na ndani ya makundi kuna hitaji la kuwa na gari imara. Baadaye ingewezekana kuwasiliana na vikundi vya KAB kwenye majimbo ya jirani ya Mbinga na Njombe na kuanza ushirikiano wa „kitaifa.“
Imepangwa sasa kwamba katibu Dieter Lwambano ashiriki katika warsha kwa viongozi huko Uganda.

Katika warsha ya viongozi wa vikundi (basegroups) wa jimbo la Songea walijadili pia masuala ya uzalishaji na masoko

Augsburg, 27. Julai 2006.  kadiri ya taarifa zilizoletwa na Dieter Lwambano, semina ilifanyika mjini Songea mwezi Juni 2006. Katika warsha hiyo iliyohudhuriwa wajumbe kutoka makundi ishirini, mada zifuatazo zilijadiliwa:
 

1.Mwanachama/mwanaharakati wa HAWAKASO/KAB na Kanisa leo. Mzungumzaji: Fr. Castor Goliama
2.Matatizo ya UKIMWI. Mzungumzaji: Daktari Komba, kutoka hospitali ya Peramiho
3.Historia ya KAB. Mzungumzaji: Katibu wa HAWAKASO jimbo Dieter Lwambano
4.Uzalishaji na masoko. Msemaji: Imani Mkwama, kutoka ofisi za serikali

Hotuba ya ufunguzi ilitolewa na Naibu wa Askofu Mkuu Fr. Reginald Moyo. Wazungumzaji wote walifanya kazi nzuri na gharama zote za warsha hiyo zitalipwa kutoka kwenye mfuko wa kazi za kimataifa wa jimbo la Augsburg.
 
Siku ya tatu ulifanyika mkutano wa jimbo pamoja na viongozi wapya waliochaguliwa. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa kama ifuatavyo:
Bertha Kapinga na Cyprian Fussi ni wenyeviti. Makatibu wawili ambao ni Theresia Hokororo na Lukas Geho. Mhasibu ni Benedict Kapinga. Kama ilivyokuwa mpaka sasa naibu wa Akofu Fr. Reginald Moyo ni mkurugenzi na Dieter Lwambano ni katibu.
 


Ni vema kutokufa moyo
Shughuli za kimataifa za KAB zinaendelea kuvuka mipaka. Ripoti ya kazi za «mpango wa kimataifa» za KAB zinapatikana katika ukurasa maalumu wa «Augsburger Kontakts» kama PDF yanye uzito wa 37 KB.
 

Songea inaendelea! Shughuli za uundaji wa ushirikiano huo bado zinaendelea.
 Tulishangazwa kupokea bahasha moja nzito, kwa njia ya posta, kutoka kwa marafiki zetu wa Songea. Dieter Lwambano, katibu wa HAWAKASO alituletea ripoti ambayo, mpaka sasa, ni ndefu na ya kina kabisa juu ya makundi yaliyo bado hai katika Jimbo Kuu la Songea. Kwa kupitia misaada ya kifedha  waipatayo toka kwetu, mambo kwa sasa yanakwenda murua.
 
Kutokana na ukosefu wa fedha ndogo ndogo za kupanua shughuli za makundi, sasa ndugu zetu hao waafrika wanapanga kuanzisha mradi mmoja wa mikopo midogo midogo kwa ajili ya makundi na wametuomba kuuwezesha mradi huo kifedha. Katika sherehe za kuadhimisha siku ya Jimbo, kama mwanzo tu wa kuwasaidia ndugu zetu hao tuliuza «Goldstucken» (fedha za cheke cheke za dhahabu bandia ambazo watu walizinunua kiishala tu ili kuweza kutoa mchango wao kwa mradi huo). Mipango ya maombi kwa mfuko huo itafanywa kupitia «weltnetwork». Apendaye kusaidia shughuli hizo za ujenzi, binafsi au kama KAB, zifanyikazo Kusini magharibi mwa Tanzania, anaweza kuwasiliana na katibu wa KAB. Zaidi...
 
Ewald Lorenz-Haggenmueler,
Mtendaji kimataifa
 


Yuro 500 zimekusanywa
KAB inasaidia mradi  wa HAWAKASO huko Songea na huko augsbug utafanyika mkutano tar. 13. Oktoba 2005. Mwishoni wa mwezi Septemba yataletwa mwa mara ya kwanza maombi toka Songea ya kuomba msaada wa kuuwezesha mradi wa mikopo midogo midogo kwa makundi. BarbaraBarbara Haggenmueller katika mkutano wa kuadhimisha siku ya Jimbo huko Senden alitujulisha juu ya mradi huo. Wahusika katika shughuli za kimataifa waligawa, katika mkutano huo, «soli-Goldtaler» na papo hapo kujivunia 500â‚. Kwa kushirikiana na «weltnotwerk» KAB inafanya mipango ya kuwasilisha msaada huo. « kweli kabisa, «leo ni leo asemaye kesho....» sisi leo hii tunawasaidia marafiki zetu wa Songea», alisema Barbara Haggenmueller. Misaada hiyo itawaimarisha wanachama. Huu ni msaada wa kujisaidia, fedha zikopeshwazo baadaye zitarudishwa katika mfuko wa chama katika ngazi ya jimbo.
Apendaye kusaidia mafanikisho ya haraka kwa mradi huu, sasa anaweza kutoa mchango wake, alisema Alfred Brendle mwanakamati ya kimataifa. Akaunti ya mchango:  268Songea2002-dia211KAB Diozesanverband Aktion Dritte welt (jumuiya ya kijimbo kwa ajili ya ulimwengu wa tatu), Akaunti namba: 128 465, Liga bank Augsburg, BLZ 750 903 00. Risiti za shukrani kwa michango hiyo zinatolewa pia. Zaidi juu ya ushirika huo unaweza kusoma katika «Augsburger Kontakt» Na. 3/2005 au hapa kama PDF data 80KB.


Mafafanuzi kwa wasanii: PDF-fomula (140KB) hapa!
 

 
Mwisho!
Shughuli za uratibu wa KAB Songea
Tar. 1 Oktoba Dieter Lwambano, ambaye ni kiongozi wa jimbo KAB DieterLwambano_a02Songea, alianza kufanya kazi kama mwajiriwa. Kadiri ya mapendekezo yetu na kwa msaada wetu Dieter Lwambano kwa kipindi cha mwaka mmoja alitakiwa kufanya kazi kama katibu wa KAB. Shughuli zke zilikuwa ni pamoja na kutembelea makundi yaliyopo, kuanzisha makundi mapya, kufanya mawasiliano na sisi pamoja na KAB ya Uganda na kumtafuta mtu ambaye angekuwa katibu. Dieter anapata mshahara wake toka «Weltnotwerk» ya KAB ya Ujerumani. Gharama za uendeshaji wa ofisi ya katibu zinapatikana katika maombi ya mradi huko Koloni.
Apendaye kusaidia gharama za uendeshaji wa ofisi hiyo, anaweza kutoa mchango wake kwa akaunti ya: KAB Diozesanverband Aktion Dritte Welt (jumuiya ya kijimbo kwa ajili ya ulimwengu wa tatu), Akaunti namba: 128 465, BLZ 750 903 00, Liga bank Augsburg. Zaidi... Data za PDF 100 KB. hivi.